Hapa kuna mifano ya mafumbo ya kuchemsha bongo na kukusaidia ufikiri zaidi:
Misemo ya mafumbo
Kulikuwa na familia moja iliyokuwa ikienda kanisani ng’ambo, na kulikuwa na daraja kubwa ya ile familia kuvuka ndiposa wawe wamefika katika kanisa hilo, ila kwenye daraja hilo chui alikuwa amelala katikati, na familia hiyo ilikuwa tu na haja ya kuhudhuria ibada ya siku hiyo, swali ni je wangefanyaje ndiposa wapite kwenye daraja hiyo iliyokuwa na chui?
Ni cheupe kama theluji, cheusi kama makaa, kina manyoya, wanaume hukiona mara tatu kwa siku na wanawake hukiona mara moja maishani mwao…jina lake lina herufi 5. Je ni kitu gani?
Palikuwa na Bw. James na punda watatu akitaka kuvuka mto mkubwa, punda wa kwanza alitaka kula nguo za Bw. James, punda wa pili alitaka kula mwili wa Bw. James, punda wa mwisho alitaka kula punda wa pili, je Bw. James alivuka vipi kwa kutumia hawa punda?
Kulikuwa na mashua ambayo ilikuwa inabeba uzito wa kilo hamsini. Mama mmoja akaenda kuvukisha ng’ombe wake, wakapima yule ng’ombe akawa na kilo hamsini. Cha majabu, mashua ilipofika katikati ya bahari, ng’ombe akajisaidia ndani ya mashua. Swali ni Je, mashua ilizama au la?
Kuna mtu alienda akanunua dawa ya panya na alipofika nyumbani akararua ile karatasi kwa kutumia wembe na akaenda akanawa mikono kwa maji ya tap. Alipopewa chakula akala na baadaye akafa…je? Ni nini kilichomuua?
Malkia aliabiri ndege kutoka Mombasa hadi Nairobi, alipofika Nairobi hakumwona dereva wa ndege lile unafikiri ni kwanini akumwona dereva?
Ndege ilianguka mpakani mwa Italy na Germany. Jje majeruhi walizikwa wapi? Italy ama Germany?
Baba alikuwa akisafiri na mifugo: Simba, Ng’ombe, na Nyasi. Alifika mtoni akapata boti linaloweza kumvusha yeye na mfugo mmoja tu kwa wakati. Je, ataanza kuvusha nini na kumalizia na nini?
Watu watatu walitaka kuvuka mto. Mmoja alikanyaga maji, wa pili aliyaona maji lakini hakuyakanyaga, na wa tatu hakuyaona wala kuyakanyaga. Hao ni akina nani?
Muislamu mmoja mtu mzima husali sala tano kwa siku. Je, Waislamu watatu watu wazima na mtoto mmoja mdogo watasali sala ngapi kwa siku mbili?
Kulikuwa na mwajiriwa wa kulinda usiku. Siku moja, bosi wake alipanga safari ya kwenda mahali kwa ndege. Mlinzi akamwambia bosi wake asisafiri kwa sababu ameota ndege itaungua. Baada ya wiki tatu, mwajiriwa akafutwa kazi. Swali ni, kwa nini alifutwa kazi?
Nina nyanya mgonjwa, na dawa ni asali inayouzwa shilingi 3. Shilingi 1 ni ya kulipa langoni unapoingia, shilingi 2 ni ya kununua asali, na shilingi 3 ni ya kulipa langoni unapotoka. Je, nifanyeje ili nimnunulie nyanya yangu asali, wakati nina shilingi mbili tu?
Wenye werevu watafumbua fumbo hili: Kuna mtoto wa mfalme juu ya mti, lakini hasemi. Mwenye kumfanya aseme atapata zawadi kubwa sana. Chini ya mti huo kuna mbuzi, nyasi, mbwa na nyama. Je, utafanyaje mpaka mtoto aseme?
Niko na kondoo wangu, na ninataka nimchinje na nile nyama yake kwa miaka miwili. Je, nifanyeje ili nyama isiharibike au kuoza kabla ya miaka miwili?
Baba Vero alinunua ndizi mbili sokoni kumletea Vero. Alipofika nyumbani, alimpata Vero akicheza na majirani wawili. Je, angefanyaje ili Vero apate ndizi moja na majirani nao wapate ndizi?
Kulikuwa na ndege kumi mtini. Nikarusha jiwe nikamgonga ndege mmoja. Je, walibaki ndege wangapi mtini?
Kulikuwa na mzee mmoja mkulima. Siku moja, akiwa kazini, alipika ugali na kitoweo. Ugali ulipoiva, aliweka kando na kuweka kitoweo jikoni. Alisahau kufunga mlango, na mbwa akala kitoweo chote. Unadhani mzee alitumia nini kula ugali?