Katika makala haya tumekupa mismeo 100 ya wahenga kupitia kwa methali.
Methali za wahenga
- Ajali haina kinga
- Ajizi ni nyumba ya njaa
- Akili ni mali, akili nyingi huondoa maarifa
- Akili ni nywele kila mtu ana zake
- Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
- Akutendaye mtende,mche asiyekutenda
- Aliye juu mngoje chini
- Aliye kando haangukiwi na mti
- Aliyekunyoa shungi kakupunguzia kuchana
- Aliyetota hajui kutota
- Baniani mbaya kiatu chake dawa
- Bao nene si chuma chembamba
- Bendera hufuata upepo
- Bilashi, bilashi, katu haitoshi
- Binadamu ni kama kilihafu hakosi uchafu
- Bura yangu sibadili kwa rehani
- Chanda chema huvikwa pete
- Chovya chovya humaliza buyu la asali
- Chungu kidogo huchemka upesi
- Dawa ya moto ni moto
- Debe shinda haliachi kutika
- Debe tupu haliachi kuvuma
- Domo kaya samli kwa mwenye ng’ombe
- Dondandugu halina dawa
- Dua la kuku halimpati mwewe
- Dunia hadaa ulimwengu shujaa
- Eda ni ada yenye faida
- Fadhila mpe mama na Mola atakubariki
- Fadhila za punda mashuzi
- Fadhili ukitenda usingoje shukrani; ukiten…
- Fahali wawili hawakai zizi moja
- Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno
- Ghururi na binadamu hawaachani
- Haba na haba hujaza kibaba
- Hadhari kabla ya hatari
- Hakuna bamvua lisilo usubi
- Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha
- Hakuna masika yasiyo na mbu
- Hakuna ziada mbovu
- Hukutia mtu wako
- Ibilisi wa mtu ni mtu
- Inuka twende ni kwa waaganao
- Ivushayo ni mbovu
- Jambo la ukucha halichukuliwi shoka
- Jaribu huleta fanaka
- Jawabu la kesho andaa leo
- Jawabu wakatiwe na wakatiwe si zani
- Jimbi wa shamba hawiki mjini
- Jino liking’oka ukubwani halimei tena
- Jogoo likiwika ama lisiwikae kutakucha
- Jogoo wa shamba hawiki miini
- Kichwa cha kuku hakihimili kilemba
- Kidole kimoja hakivunji chawa
- Kifo cha wengi harusi
- Kila mtoto na koja lake
- Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta kwake
- Kila ndege huruka kwa ubawa wake
- Kilichoingia mjini si haramu
- Kimya kingi kina mshindo mkuu
- Kivuli cha mgude husaidia walio mbali
- Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele
- Kukopa harusi kulipa matanga
- Kuku havunji yai lake
- Kuku mgeni zawadi za kunguru
- Kula kutamu kulima mavune
- Kula ni vyepesi lakini kulima ng’o
- Kula uhondo kwataka matendo
- Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana
- Kunguru mwoga hukimbiza bawa lake
- Kutoa ni moyo si utajiri
- Kutoa ni moyo usambo ni utajiri
- Kuzimika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi
- Kwenye udongo hukosi mfinyanzi
- La kuvunda halina ubani
- La mgambo likilia kuna jambo
- Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo
- Lila na fila havitangamani
- Lililompata peku na ungo litampata
- Linalopita hupishwa, yaliyopita si ndwele tena
- Maji mafu mvuvi kafu
- Maji ya nazi hutafuta mvungulio
- Majuto ni mjukuu huja baada ya kitendo
- Makuukuu ya mwewe si mapya ya kengewa
- Mali bila daftari hupotea bila habari
- Mali ilivunja nguu milima ikalala
- Mali ya bahili huliwa na mchwa
- Mama mkwe hafungui mdomo
- Mambo kangaja huenda yakaja
- Mashua ya maskini huzama mtoni
- Maskini hana kinyongo
- Maskini hana rafiki
- Maskini haokoti, akiokota huambiwa keba
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni
- Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake
- Mchovya asali hachovyi mara moja
- Mdomo siri ya gunda
- Meno ya mbwa hayaumani
- Mfa maji haishi kutapatapa
- Mficha uchi hazai
- Mfinyanzi hulia gaeni
- Mgaagaa na upwa hali wali mkavu
- Mganga hajigangi
- Mgema akisifiwa tembo hulitia maji